Date: 
30-03-2022
Reading: 
1Wakorintho 10:17-22

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi tarehe 30.03.2022

1 Wakorintho 10:17-22

17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.

18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu?

19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?

20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.

21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?

Yesu ni mkate wa uzima;

Mtume Paulo anawaandikia waKorintho kuhusu ushirika katika Sakramenti ya madhabahu, yaani ushirika wa meza ya Bwana. Anawaalika waKorintho kushiriki inavyostahili ili wasiingie hukumuni. 

Mtume Paulo anatukumbusha kuwa sisi sote twashiriki mkate mmoja na kunywea kikombe kimoja. Tafsiri yake ni kuwa Yesu alikuja kutuokoa sote. Hivyo wewe na mimi tunao wajibu wa kumwamini na kumpokea Yesu aliyetuokoa kwa njia ya kifo msalabani, kwa ajili maisha ya sasa na hata uzima wa milele, maana yeye ndiye mkate wa uzima.

Siku njema.