Date: 
08-07-2020
Reading: 
1Samuel 3:15-21

WEDNESDAY 20TH MAY 2020  MORNING                                                   

1Samuel 3:15-21  New International Version (NIV)

15 Samuel lay down until morning and then opened the doors of the house of the Lord. He was afraid to tell Eli the vision, 16 but Eli called him and said, “Samuel, my son.”

Samuel answered, “Here I am.”

17 “What was it he said to you?” Eli asked. “Do not hide it from me. May God deal with you, be it ever so severely, if you hide from me anything he told you.” 18 So Samuel told him everything, hiding nothing from him. Then Eli said, “He is the Lord; let him do what is good in his eyes.”

19 The Lord was with Samuel as he grew up, and he let none of Samuel’s words fall to the ground. 20 And all Israel from Dan to Beersheba recognized that Samuel was attested as a prophet of the Lord. 21 The Lord continued to appear at Shiloh, and there he revealed himself to Samuel through his word.

It is always the responsibility of God's messenger to bring everything God says, not just the "easy" words. The result of sin and unbelief in others will fall on us if we do not warn them.


JUMATANO TAREHE 8 JULAI 2020  ASUBUHI                                             

1SAMWELI 3:15-21

15 Naye Samweli akalala hata asubuhi, akaifungua milango ya nyumba ya Bwana. Samweli akaogopa kumjulisha Eli maono hayo.
16 Basi Eli akamwita Samweli, akasema, Samweli, mwanangu. Naye akajibu, Mimi hapa.
17 Akamwuliza, Ni neno gani alilosema nawe? Nakusihi, usinifiche; Mungu akufanyie vivyo hivyo, na kuzidi, ukinificha lo lote katika hayo yote Bwana aliyosema nawe.
18 Basi Samweli akamwambia kila neno, asimfiche lo lote. Naye akasema, Ndiye Bwana; na afanye alionalo kuwa ni jema.
19 Samweli akakua, naye Bwana alikuwa pamoja naye, wala hakuliacha neno lake lo lote lianguke chini.
20 Nao Waisraeli wote, toka Dani mpaka Beer-sheba, walitambua ya kwamba huyo Samweli amewekwa kuwa nabii wa Bwana.
21 Naye Bwana akaonekana tena huko Shilo; kwa kuwa Bwana akajifunua kwa Samweli huko Shilo, kwa neno la Bwana. Nalo neno la Samweli likawajia Israeli wote.

Ni wajibu wa watumishi wa Mungu kila wakati kuleta ujumbe wa Mungu kama alivyowaagiza, na siyo maneno matamu tu. Matokeo ya dhambi na kutoamini kwa wengine yatakuwa juu yetu ikiwa hatutachukua nafasi kuwaonya.