Date: 
21-04-2021
Reading: 
1Peter 5:1-4

WEDNESDAY 21ST APRIL 2021   MORNING                                     

1Peter 5:1-4 New International Version (NIV)

To the elders among you, I appeal as a fellow elder and a witness of Christ’s sufferings who also will share in the glory to be revealed: Be shepherds of God’s flock that is under your care, watching over them—not because you must, but because you are willing, as God wants you to be; not pursuing dishonest gain, but eager to serve; not lording it over those entrusted to you, but being examples to the flock. And when the Chief Shepherd appears, you will receive the crown of glory that will never fade away.

This call is for us, to exercise watch and care over God's people entrusted under our care, to encourage and shepherd them in a godly direction from a godly example. Leadership is never about what we get out of it or a force of our will; rather, it is about the mobilization of His teachings from His Word in our life so that it flows onto others lives.  Let us eagerly seek to know Him more powerfully so we can serve with more humility.


JUMATANO TAREHE 21 APRILI 202I   ASUBUHI                       

1 PETRO 5:1-4

1 Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;
2 lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.
3 Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.
4 Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.

Wito huu ni kwa ajili yetu, kuchunga na kuwatunza watu wote ambao  Mungu ameweka chini yetu, kuwatia moyo na kuwaongoza katika mfano na uelekeo ule ambao Mungu anatuelekeza. Uongozi siyo kwa ajili ya kujipatia faida au kujilazimisha; bali ni kupokea mafundisho toka katika neno la Mungu ili yaweze kuleta badiliko katika maisha yetu na baadaye kwa wengine. Basi, tumtafute Mungu kwa bidii na kwa nguvu zetu zote ili tuweze kumtumikia kwa unyenyekevu.