Date: 
27-01-2021
Reading: 
1Corinthians 3:1-9

WEDNESDAY 27TH JANUARY 2021  MORNING                                        

1Corinthians 3:1-9 New International Version (NIV)

Brothers and sisters, I could not address you as people who live by the Spirit but as people who are still worldly—mere infants in Christ. I gave you milk, not solid food, for you were not yet ready for it. Indeed, you are still not ready. You are still worldly. For since there is jealousy and quarreling among you, are you not worldly? Are you not acting like mere humans? For when one says, “I follow Paul,” and another, “I follow Apollos,” are you not mere human beings?

What, after all, is Apollos? And what is Paul? Only servants, through whom you came to believe—as the Lord has assigned to each his task. I planted the seed, Apollos watered it, but God has been making it grow. So neither the one who plants nor the one who waters is anything, but only God, who makes things grow. The one who plants and the one who waters have one purpose, and they will each be rewarded according to their own labor. For we are co-workers in God’s service; you are God’s field, God’s building.

In the ministry of Jesus, what we do is important. However, we are not the focus. We are only servants. We are God’s fellow workers; we are his field, not ours. We are his building, not ours. We are servants, ministers.


JUMATANO TAREHE 27 JANUARY 2021  ASUBUHI                  

1WAKORINTHO 3:1-9

1Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.
Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi,
kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?
Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?
Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.
Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.
Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.
Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.
Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.

Katika huduma ya Yesu, tunachofanya ni muhimu. Hata hivyo, sisi siyo walengwa. Sisi tu watumishi tu. Sisi ni watenda kazi pamoja na Mungu; sisi ni shamba lake, siyo letu. Sisi ni jingo lake, siyo mali yetu. Sisi tu watumishi, wahudumu.