Date: 
30-11-2019
Reading: 
1Corinthians 15:24-28 (1Korintho 15:24-28)

SATURDAY 30TH NOVEMBER 2019  MORNING   1Timothy 15:24-28
1 Corinthians 15:24-28 New International Version (NIV)

24 Then the end will come, when he hands over the kingdom to God the Father after he has destroyed all dominion, authority and power. 25 For he must reign until he has put all his enemies under his feet. 26 The last enemy to be destroyed is death. 27 For he “has put everything under his feet.”[c] Now when it says that “everything” has been put under him, it is clear that this does not include God himself, who put everything under Christ. 28 When he has done this, then the Son himself will be made subject to him who put everything under him, so that God may be all in all.

At the end of this physical life, there is a spiritual life, which continues forever, a life with the creator of the universe. Therefore, our choice to believe and then live out what we believe relates to the next life.  Every one of us must make a choice about where their Spirit will spend the rest of eternity.


ALHAMISI TAREHE 30 NOVEMBA 2019 ASUBUHI               1WAKORINTHO 15:24-28
24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.


Mwisho wa maisha haya ya kimwili, ni mwanzo wa maisha ya kiroho, ambayo yataendelea milele, kuishi pamoja na muumbaji wa ulimwengu. Hivyo basi, uchaguzi wa kuamini na kuishi kile tunachoamini vina uhusiano wa moja kwa moja na maisha yajayo.  Kila mmoja wetu ni lazima achague mahali ambapo roho yake itakaa milele.