Date: 
06-12-2021
Reading: 
1 Wathesalonike 5:1-5

Hii ni Advent 

Jumatatu asubuhi tarehe 06.12.2021

1 Wathesalonike 5:1-5

[1]Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

[2]Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

[3]Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

[4]Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

[5]Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

Bwana anakuja katika Ufalme wake;

Mtume Paulo anawaandikia Wathesalonike kuwa tayari kumpokea Bwana, ambaye atakuja kama mwizi. Mwizi hana mihadi, huvamia ghafla! Hapa ujumbe wa Mtume Paulo ni kuwa hatujui siku wala saa Bwana atakaporudi, hivyo kujiandaa muhimu.

Ujumbe huu unakuja kwetu Jumatatu ya leo, kutukumbusha kuwa Yesu atarudi siku tusiyoijua, hivyo tuwe tayari wakati wote kumpokea. Jiandae kumpokea Bwana, siku isiyojulikana atarudi. 

Uwe na wiki njema yenye ushuhuda na mafanikio.