Date: 
20-09-2018
Reading: 
1 Timothy 4:1-5

THURSDAY 20TH SEPTEMBER 2018 MORNING                        

1 Timothy 4:1-5 New International Version (NIV)

 

1 The Spirit clearly says that in later times some will abandon the faith and follow deceiving spirits and things taught by demons. Such teachings come through hypocritical liars, whose consciences have been seared as with a hot iron. They forbid people to marry and order them to abstain from certain foods, which God created to be received with thanksgiving by those who believe and who know the truth. For everything God created is good, and nothing is to be rejected if it is received with thanksgiving, because it is consecrated by the word of God and prayer.

There are many warnings in the Bible about false teachers and false prophets. We need to be careful that we are not deceived. We should check any teachings against God’s Word in the Bible and not take any verse out of its context. The most important teachings are always repeated in several different places in the Bible so that we should not miss them.

ALHAMISI TAREHE  20 SEPTEMBA 2018 ASUBUHI                      

1 TIMOTHEO 4:1-5

1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 
kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 
wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. 
Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 
kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. 

Kuna maonyo mengi katika Biblia kuhusu walimu na manabii ya uongo. Tujitahadari tusidanganywe. Tusikubali tu mafundisho yote bila kulinganisha na Neno la Mungu katika Biblia. Pia ni hatari kutoa mstari mmoja bila kuangalia mazingira yake. Mafundisho ya muhimu zaidi yanajirudia rudia katika sehemu nyingi za Biblia ili tusikose.