Date: 
31-10-2022
Reading: 
1 Timotheo 6:11-16

Jumatatu asubuhi tarehe 31.10.2022

1 Timotheo 6:11-16

[11]Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.

[12]Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.

[13]Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato,

[14]kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;

[15]ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;

[16]ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.

Ushuhuda wetu; Hapa nimesimama;

Mtume Paulo anamwandikia Timotheo akimtaka kupiga vita vya Imani. Anamsihi kudumu katika utume wake kama alivyoitwa akiwa mwenye haki, imani, saburi, utauwa, upendo na upole. Paulo anamtaka Timotheo kumtumikia Mungu kwa uaminifu ambaye atamdhihirisha mbele ya kiti cha enzi. 

Kupiga vita vizuri vya Imani ni kuenenda kama tulivyoitwa pale tulipompokea Yesu. Ni kutimiza wajibu wetu tukitenda mema na kuepuka mafundisho yasiyofaa. Yesu Kristo aliyetuita anatutaka kuvipiga vita vizuri vya Imani akituahidi kutudhihirisha kwenye uzima wa milele. 

Uwe na wiki njema yenye ushuhuda.