Date: 
14-10-2022
Reading: 
1 Timotheo 4:1-5

Ijumaa asubuhi tarehe 14.10.2022

1 Timotheo 4:1-5

1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;

5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.

Kristo ametuweka huru;

Mtume Paulo anamwandikia Timotheo kuhusu waaminio roho zidanganyazo. Hii anaiita kujitenga na Imani! Anaandika juu ya walimu wa uongo, akiita mafundisho yao "mafundisho ya mashetani". Walimu hawa hufundisha kwa kupotosha neno la Mungu wakiwaelekeza watu kufanya isivyostahili. Kumbe walimu hawa hulipoteza kundi la Mungu.

Mtume Paulo anamsisitiza Timotheo kudumu katika imani akifundisha kweli ya Mungu;

1 Timotheo 4:16 Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.

Ujumbe huu unatukumbusha kuwa makini na mafundisho yasiyofaa. Tuwaepuke walimu wa uongo maana siku hizi wako wengi. Tuendelee kukaa katika Bwana kama tulivyoitwa, msingi wetu ukiwa ni neno la Mungu, na Yesu Kristo aliye msingi wa Kanisa atatupa mwisho mwema.

Nakutakia mapumziko mema.