Date: 
15-03-2022
Reading: 
1 Samweli 20:31-34

Hii ni Kwaresma

Jumanne asubuhi tarehe 15.02.2022

1 Samweli 20:31-34

31 Maana wakati mwana wa Yese akiwa hai juu ya nchi, wewe hutafanikiwa, wala ufalme wako. Basi, sasa peleka, ukamlete kwangu, maana hakika yake atakufa huyu.

32 Yonathani akamjibu Sauli, baba yake, akamwambia, Auawe kwa sababu gani? Amefanya nini?

33 Sauli akamtupia mkuki wake ili kumpiga; basi Yonathani akajua ya kuwa baba yake ameazimu kumwua Daudi.

34 Basi Yonathani akaondoka pale mezani, mwenye hasira kali, wala hakula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi sana, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.

Tupinge ukatili;

Sauli alikuwa akitaka kumuua Daudi. Hakufurahishwa na ushujaa wake, kwa mengi aliyofanya ikiwemo kumuua Goliath. Ukisoma nyuma kidogo, unaweza kuona hapa;

1 Samweli 18:7-9

7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.
 
8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme?
 
9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.

Sauli ni wazi alikuwa roho mbaya, kwa alichoonesha kwa Daudi. Tunaalikwa asubuhi hii kuacha roho mbaya. Tusione wivu kwa mafanikio ya wenzetu, bali tutiane moyo na kusaidiana, ili tumtumikie Mungu wetu kwa pamoja.

Siku njema.