Date: 
18-01-2022
Reading: 
1 Samweli 1:1-11

Jumanne asubuhi tarehe 18.01.2022

1 Samweli 1:1-11

1 Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu

2 naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto.

3 Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea Bwana wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa Bwana, walikuwako huko.

4 Hata siku ile ilipofika Elkana alipotoa dhabihu, kumpa mkewe Penina sehemu, akawapa na watoto wake wote, waume kwa wake, sehemu zao;

5 lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo.

6 Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo.

7 Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa Bwana, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula.

8 Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi?

9 Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la Bwana.

10 Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana.

11 Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.

Mungu hutakasa nyumba zetu;

Elkana alikuwa na wake wawili, Hana na Penina. Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto, kitendo kilichosababisha hata mke mwenzie (Penina) kumcheka. Hana anaweka nadhiri kuwa akipata mtoto atamtoaa kwa Bwana maisha yake yote. Ukiendelea kusoma unaona Hana alipata mtoto, ndiye Samweli.

Kutokuwa na mtoto hakumzuia Hana kudumu hekaluni akisali siku zote. Imani yake ilizidi hadi kumtolea Mungu nadhiri, hadi akapata mtoto. Ni kwa kiasi gani unamtegemea Mungu katika nyakati unazopitia? Usikate tamaa katika hali yoyote, mtegemee Kristo, naye atakubariki. Atakutakasa.

Mungu hutakasa nyumba zetu.

Siku njema.