Date: 
21-02-2022
Reading: 
Yoshua 1:8-9

Jumatatu asubuhi tarehe 21.02.2022

Yoshua 1:8-9

8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.

Neno la Mungu lina nguvu;

Baada ya Musa kufa, Mungu alimpa Yoshua maelekezo ya kuwaongoza wana wa Israeli kuelekea nchi ya ahadi. Anamwambia asiiache torati, akitenda sawa na maelekezo toka kwa Mungu. 

Kwa sasa naweza kusema Yesu anatuamuru kuwa neno lake lisiondoke vinywani mwetu. Anatuita kumfuata tukilishika neno lake, ili lituongoze kutenda sawasawa na mapenzi yake. Hapo ndipo Yesu anatuambia tusiogope, maana yuko nasi popote tuendako.

Uwe na wiki njema, ukilishika neno la Mungu.