Date: 
16-02-2022
Reading: 
Yohana 6:37-49

Jumatano asubuhi tarehe 16.02.2022

Yohana 6:37-40

37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.

38 Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.

39 Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho.

40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Tunaokolewa kwa neema

Yesu alisema kwamba hakutoka mbinguni ili afanye mapenzi yake, bali mapenzi yake Mungu, kwamba wote wajao kwake waokolewe, wasipotee. Mapenzi haya ni kuokoa wanadamu, ili wote waurithi uzima wa milele.

Yesu anaonesha kuwa hakuna mwanadamu aliyeomba kuokolewa, bali ni Mungu aliyeleta wokovu bure, kwa neema. Yesu anaonesha kuwa yuko tayari, anatungojea twende kwake atuokoe maana ndiyo kazi iliyomleta. Unasubiri nini?

Siku njema.