Date: 
18-03-2021
Reading: 
Yohana 6:26-31

JUMATANO TAREHE 18 MACHI 2021, ASUBUHI.

Yohana 6:26-31 Neno: Bibilia Takatifu

26 Yesu akawajibu, “Ni wazi kwamba ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza ninayofanya, isipo kuwa mnanitafuta kwa sababu mlikula mikate mkashiba. 27 Msishug hulikie sana chakula kiharibikacho bali shughulikieni chakula kidumucho; chakula cha uzima wa milele. Chakula hicho, nitawapeni mimi Mwana wa Adamu, ambaye Baba Mungu mwenyewe amenithibit isha.”

28 Wakamwuliza, “Tufanye nini ili tuonekane kuwa tunatenda kazi ya Mungu?”

Read full chapter

Yesu ni chakula cha uzima;

Yesu anawaambia waliomfuata baada ya kushiba mikate na samaki kuwa wanamfuata kwa sababu ya mikate, na siyo kwa sababu ya ishara! Anawaambia wasikitendee kazi chakula kiharibikacho, bali kidumucho hata uzima wa milele. Yaani wamwamini Yesu, aliye chakula cha uzima.

Wito huu unatujia asubuhi ya leo, kuwa tusimfuate Yesu kwa ajili tu ya tamaa zetu, bali tumwamini na tumfuate kwa utii wa neno lake, yeye aliye chakula kisichoharibika, kwa uzima wa milele.

Alhamisi njema.


THURSDAY 18TH MARCH 2021, MORNING

John 6:26-28 New International Version

26 Jesus answered, “Very truly I tell you, you are looking for me, not because you saw the signs I performed but because you ate the loaves and had your fill. 27 Do not work for food that spoils, but for food that endures to eternal life, which the Son of Man will give you. For on him God the Father has placed his seal of approval.”

28 Then they asked him, “What must we do to do the works God requires?”

Read full chapter

Jesus is the bread of life;

Jesus tells those who have followed him after they are satisfied with bread and fish that they are following him because of the loaves, and not because of the signs! He tells them to work, not for the food that perishes, but for the life that lasts forever. That is, believe in Jesus, who is the bread of life.

This call comes to us this morning, that we should not follow Jesus only for our own desires, but that we should believe in him and follow him in obedience to his word, who is the incorruptible food, for eternal life.

Good Thursday.