Date: 
18-10-2022
Reading: 
Yeremia 33:23-28

Jumanne asubuhi tarehe 18.10.2022

Yeremia 31:23-28

[23]BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Watatumia tena neno hili katika nchi ya Yuda, na katika miji yake, nitakapowarudisha mateka yao; BWANA na akubariki, Ee kao la haki, Ee mlima wa utakatifu.

[24]Na Yuda, na miji yake yote, watakaa humo pamoja; wakulima, nao waendao huko na huko pamoja na makundi yao.

[25]Kwa maana nimeishibisha roho yenye uchovu, nami nimeiridhisha kila roho yenye huzuni.

[26]Basi, nikaamka, nikaangalia; na usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu.

[27]Tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapoipanda nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, mbegu ya mwanadamu na mbegu ya mnyama.

[28]Tena itakuwa, kwa kadiri nilivyowaangalia, ili kung’oa, na kubomoa, na kuangusha, na kuangamiza, na kutesa; kwa kadiri iyo hiyo nitawaangalia, ili kujenga, na kupanda, asema BWANA.

Upendo wa kweli watoka kwa Mungu;

Ni utabiri wa Nabii Yeremia juu ya Taifa la Israel kurejeshwa toka mateka. Alitumwa kuleta ujumbe wa ukombozi kwa Taifa la Mungu kuwa wangekombolewa na kukaa katika kao lao kwa utakatifu. Israeli waliahidiwa kukaa katika nchi yao na makundi yao yote. 

Kwa kurudishwa kwenye nchi yao, Mungu alikuwa upande wa Israeli. Hakutaka wakae milele utumwani wakiwa mateka.

Tabia ya Mungu ni upendo, ndiyo maana alimtuma Yesu Kristo afe kwa ajili yetu kutukomboa na dhambi. Kwa upendo wa Mungu tumekombolewa. Tuuishi upendo huu kwa kutenda mema.

Siku njema.