Date: 
14-01-2022
Reading: 
Yeremia 32:40-32

Ijumaa asubuhi tarehe 14.01.2022

Yeremia 32:40-42

40 nami nitafanya agano la milele pamoja nao, kwamba sitageuka wala kuwaacha, ili niwatendee mema; nami nitatia kicho changu mioyoni mwao, ili wasiniache.

41 Naam, nitafurahi juu yao niwatendee mema, nami nitawapanda katika nchi hii kweli kweli, kwa moyo wangu wote, na kwa roho yangu yote.

42 Maana Bwana asema hivi, Kama nilivyoleta mabaya makuu haya yote juu ya watu hawa, vivyo hivyo nitaleta juu yao mema hayo yote niliyowaahidia.

Wabatizwao ndio wana wa Mungu;

Yeremia anatumwa kuleta ujumbe wa Agano toka kwa Bwana kutowaacha watu wake, akiahidi kuwatendea mema siku zote. Bwana anaahidi kufurahi na watu wake, na wao kujaa furaha katika yeye, akitimiza ahadi zake kwao.

Agano la Mungu limetimia kwetu kwa njia ya ubatizo ambapo tunapata msamaha wa dhambi kuelekea uzima wa milele. Kwa maana hiyo Bwana hajatuacha. Nasi tudumu katika ahadi ya kuwa na Bwana kwa kuuishi ubatizo wetu, ili ahadi zake zitimie kwetu na hatimaye uzima wa milele.

Ijumaa njema.