Ijumaa asubuhi tarehe 05.08.2022
Warumi 7:7-13
7 Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.
8 Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.
9 Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa.
10 Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti.
11 Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, na kwa hiyo ikaniua.
12 Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.
13 Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.
Mungu amejaa neema inayotuwezesha;
Sheria inaweza kumlinda mtu akiwa hai. Mfano, mwanandoa mmoja akifariki, aliyebaki huruhusiwa kuwa na ndoa nyingine. Aliyekufa anakutana na Mungu kwa hesabu ya uwakilj wake. Mtume Paulo anawaambia Warumi kuwa wameifia torati kwa njia ya mwili wa Kristo, wawe mali yake aliyefufuka katika wafu.
Sheria husaidia kutambua dhambi. Na njia ya kuishinda dhambi ni kwa msaada wa Mungu. Hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria, kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria. Tutakuwa wenye haki kwa njia ya Imani. Tumekombolewa bure kwa njia ya ukombozi uliomo katika Yesu Kristo. Mtegemee Mungu kwa imani ili uwe na mwisho mwema.
Siku njema.