Date: 
25-03-2021
Reading: 
Warumi 5:8-11 (Romans 5:8-11)

ALHAMISI TAREHE 25 MACHI 2021, ASUBUHI

Warumi 5:8-11  Neno: Bibilia Takatifu

Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo ali kufa kwa ajili yetu.

Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa damu yake, bila shaka atatuokoa kutoka katika ghadhabu ya Mungu. 10 Kwa kuwa kama tulipokuwa maadui wa Mungu tulipatanishwa kwa kifo cha Mwanae, bila shaka sasa kwa kuwa tumepatanishwa, tutaokolewa kwa uzima wake. 11 Si hivyo tu, bali pia tunamfurahia Mungu katika Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa ajili yake tumepokea upatanisho wetu.

Read full chapter

Yesu ni mpatanishi

Mtume Paulo anawaandikia Warumi kuwa Yesu Kristo alikufa kwa ajili yetu tungali wenye dhambi. Anaongeza kuwa kwa kupatanishwa naye, tumeokolewa kuelekea uzima wa milele.

Paulo anatuhakikishia kuwa tayari tumeokolewa. Basi nakusihi tusiipoteze neema hii ya upatanisho, ili tuwe na mwisho mwema.

Siku njema.


THURSDAY 25TH MARCH 2021, MORNING

ROMANS 5:8-11

But God demonstrates his own love for us in this: While we were still sinners, Christ died for us.

Since we have now been justified by his blood, how much more shall we be saved from God’s wrath through him! 10 For if, while we were God’s enemies, we were reconciled to him through the death of his Son, how much more, having been reconciled, shall we be saved through his life! 11 Not only is this so, but we also boast in God through our Lord Jesus Christ, through whom we have now received reconciliation.

Read full chapter

Jesus is the mediator

The apostle Paul writes to the Romans that Jesus Christ died for us while we were still sinners. He adds that by being reconciled to him, we have the promise toward eternal life.

Paul assures us that we are already saved. So I beg you not to lose this grace of atonement, so that we may have a happy ending.

Good day.