Jumanne asubuhi tarehe 01.03.2022
Waefeso 3:1-10
1 Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa;
2 ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu;
3 ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache.
4 Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.
5 Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;
6 ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;
7 Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
8 Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;
9 na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote;
10 ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;
Tazameni tunapanda kwenda Yerusalemu;
Mtume Paulo anawaandikia Waefeso juu ya neema aliyopewa na Mungu kuhubiri Injili, akitangaza habari za ufalme wa Mungu. Paulo anajiona mdogo, kuliko mdogo wa watakatifu wote. Paulo anawasihi waefeso kufuatilia na kujifunza neno la Mungu lililoshushwa kwa neema, ili wakae na Kristo wakati wote.
Ujumbe wa Paulo asubuhi hii ni kuishi na Kristo maisha yote, ili tuwe na hatma njema tukiongozwa na Kristo mwenyewe. Tuwe na ujasiri maana kwa njia ya Kristo tunaokolewa, na hatma yetu ni Kristo mwenyewe.
Siku njema