Date: 
09-06-2021
Reading: 
Waebrania 10:23-25 (Hebrews 10:23-25)

JUMATANO TAREHE 9 JUNI 2021, ASUBUHI

Waebrania 10:23-25

23 Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu;
24 tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;
25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Mungu au Ulimwengu;

Leo asubuhi tunakumbushwa kuwa wavumilivu katika maisha yetu ya ufuasi. Uvumilivu huu ni kudumu katika Imani bila kuchoka tukitenda yatupasayo. Neno linatusisitiza kuhimizana katika upendo, ili nguvu ya Mungu isiondoke kwetu.

Mstari wa 25 unatuhusia kuwa tuendelee kukusanyika, tukifundishana na kuonyana kadri itupasavyo.

Ujumbe mkuu wa asubuhi ya leo ni kuwa wavumilivu katika safari ya Imani, yaani kudumu katika kweli ya Mungu, ili tuwe wa Mungu mwenyewe, na siyo ulimwengu.

Siku njema.


WEDNESDAY 9TH JUNE 2021, MORNING.

Hebrews 10:23-25  [NIV]

23 Let us hold unswervingly to the hope we profess, for he who promised is faithful. 24 And let us consider how we may spur one another on toward love and good deeds, 25 not giving up meeting together, as some are in the habit of doing, but encouraging one another—and all the more as you see the Day approaching.

Read full chapter

God or the Universe;

This morning we are reminded to be patient in our life of discipleship. This patience is to persevere in the Faith without ceasing to do what we ought to do. The Word urges us to encourage one another in love, so that the power of God may not depart from us.

Verse 25 tells us to keep on gathering together, teaching and admonishing one another as we should.

The main message of this morning is to be patient in the journey of faith, that is, to abide in the truth of God, so that we may belong to God Himself, and not to the world.

Good day.