Date: 
09-12-2022
Reading: 
Ufunuo wa Yohana 3:7-10

Hii ni Advent 

Ijumaa asubuhi tarehe 09.12.2022

Ufunuo wa Yohana 3:7-10

7 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.

8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.

9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.

10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

Bwana anakuja katika Utukufu wake;

Bwana huyaona matendo ya watu wake, huwaona na kuwapokea wote wanaomwamini. Huu ni Ufunuo aliopewa Yohana kwa Kanisa la Filadelfia, ambapo msisitizo ni kulishika neno la Mungu, Mungu akiahidi kuwalinda watu wake wasiharibiwe.

Maisha tunayoishi yapo mbele za Mungu, anatuona. Hatuwezi kumficha jambo lolote. Tunawajibika kutenda yale yanayompendeza. Tutaweza, maana yeye hututia nguvu. Tutumie fursa ya wokovu kutenda mema kwa ajili ya maisha ya sasa na yajayo.

Nakutakia mapumziko mema.