Hayo yalikuwa ni maneno ya kichwa cha habari katika semina ya kiroho ya umoja wa
wanawake wa usharika wa Azania Front iliyofanyika kule Belinda Beach Resort siku ya
jumamosi tarehe 14/6/2014.
Wengi wamekuwa na fikra kwamba mwanamke kazi yake ni kulea watoto nyumbani tu,
kumbe mwanamke ana kazi nyingi ambazo ndiyo majukumu yake yampasayo kuyatenda
kila siku, kwa kifupi naweza kusema huo ni upako wa kipekee ambao mwanamke amepewa
na Mungu, kwani mungu ana mpango na kila mwanamke anayemtumikia. Pia wanawake wana
nafasi katika maombi ya kuiombea familia, kanisa na nchi. Ukiangalia kwa maisha ya kila siku,
mwanamke ndio wa kwanza kuamka na ndio wa mwisho kulala.“Wanawake wana nafasi ya kipekee
katika kanisa na niwashauri katika familia, hivyo basi wastahili kupewa nafasi ya kusikilizwa maana
mchango wao ni muhimu sana katika jamii” alisema Chaplin Charles Mzinga alipokuwa anafungua
semina ya kiroho ya siku moja iliyofanyika mjini Dar es salaam.
“Wanawake siku zote ndio wanaotetea familia, ndio maana Yesu aliwaambia wanawake kwamba,
msinililie mimi bali lieni kwa ajili ya familia zenu na watoto wenu, ukisoma kwa makini utaona
kwamba wanawake ndio waliokuwa wanapewa kipaumbele katika kila kitu, pia wanawake ndio
waliokuwa wa kwanza kujua kwamba Yesu amefufuka kutoka kaburini, inaonyesha jinsi gani
mwanamke ana nafasi katika maisha ya kila siku ya mwanadamu ” alisema Chaplin Charles Mzinga.
Naye Mnenaji katika semina hiyo Mchungaji Grace Masalakulangwa alisema’Mungu ameweka mambo
matano makubwa ya uelewa ndani ya mwanamke nayo ni ,
¦
1.Kipawa cha ushawishi na ushauri.
2.Hali ya kuthubutu ,
3.Kutatua matatizo na kutia moyo na kupatanisha
4.Uombolezaji
5.kuhakiki ustawi wa kiuchumi katika familia.
¦
Baadhi ya wanawake wakifatilia jambo kwenye semina
¦
Chaplain Charles Mzinga akifungu Semina ya Wanawake wa Azania Front
¦
Katibu Mkuu wa umoja wa wanawake wa Azania Front akiongea jambo wakati wa semina
¦
Khanga ya kumbukumbu ya Semina ya Wanawake iliyofanyika Belinda Resort mwaka 2014
¦
Makamu Mwenyekiti Bi Stella Sykes (kushoto) na Katibu Msaidizi Bi Jane Mhina wakifuatilia maombi
¦
Mama Askofu Erica Malasusa akielekea meza kuu kwenda kmkaribisha mgeni rasmi
¦
Mama Mchungaji T Kibona (kulia) akiwasalimu wanasemina
¦
Mchungaji, Mnenaji G. Masalakulangwa akiliombea kanisa na Taifa la Tanzania
¦
Msehereshaji Mama A Mzinga akisisitiza jambo
¦
Mshereheshaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu Paul Mwangosi, akitumbuiza katika Semina
¦
Mwanasemina Bi kavugha, akiwaasa wanawake na wasichana katika semina
¦
Mwasibu wa Umoja wa Uanawake Bi Elly Swai akijiandaa na semina
¦
Mwenyekiti Bi A kilewo akiwatambulisha viongozi wa Umoja wa wanawake wa Azania Front
¦
Viongozi wa Azania Front wakiwa na wageni rasmi katika picha ya pamoja
¦
Wakinamama wa kwaya ya Wanawake wa Azania Front wakiimba
¦
Wanasemina wakiomba
¦
Watoto wa kike waliohudhuria semina wakiombewa