Date: 
06-11-2019
Reading: 
Revelation 7:9-12 (Ufunuo 7:9-12)

Wednesday 6th November 2019 Morning   

Revelation 7:9-12 New International Version (NIV)

After this I looked, and there before me was a great multitude that no one could count, from every nation, tribe, people and language, standing before the throne and before the Lamb. They were wearing white robes and were holding palm branches in their hands. 10 And they cried out in a loud voice:

“Salvation belongs to our God,
who sits on the throne,
and to the Lamb.”

11 All the angels were standing around the throne and around the elders and the four living creatures. They fell down on their faces before the throne and worshiped God, 12 saying:

“Amen!
Praise and glory
and wisdom and thanks and honor
and power and strength
be to our God for ever and ever.
Amen!”

Being a Christian does not keep us from challenges of life, but rather we are enabled to go through whatever comes against us in our journey of Faith. In other words, we are not exempted from sickness, betrayals, wars and other calamities; but our participation in it signals God’s presence in our lives through and beyond this life.


JUMATANO TAREHE 6 NOVEMBA 2019 ASUBUHI                                       

UFUNUO 7:9-12

Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;
10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.
11 Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,
12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.

Kuwa Wakristo haituepushi na changamoto za maisha haya, lakini tunapewa utayari wa kupitia chochote kitakachokuja dhidi yetu katika safari yetu ya imani. Kwa maneno mengine, hatujatengwa na magonjwa, usaliti, vita na majanga mengine; isipokuwa kuhusika kwetu katika hayo kunaonesha uwepo wa Mungu katika maisha yetu ya sasa na katika ulimwengu ujao.