Date: 
08-12-2020
Reading: 
Proverbs 8:22-27 (Mithali 8:22-27)

TUESDAY 8TH DECEMBER 2020  MORNING                                

Proverbs 8:22-27 New International Version (NIV)

22 “The Lord brought me forth as the first of his works,[c][d]
    before his deeds of old;
23 I was formed long ages ago,
    at the very beginning, when the world came to be.
24 When there were no watery depths, I was given birth,
    when there were no springs overflowing with water;
25 before the mountains were settled in place,
    before the hills, I was given birth,
26 before he made the world or its fields
    or any of the dust of the earth.
27 I was there when he set the heavens in place,
    when he marked out the horizon on the face of the deep,

The Son of God declares himself to have been engaged in the creation of the world. When the world became corrupted, He became the Savior of the world, who was the Creator of it! The Son of God was ordained, before the world, to that great work. If He delights in saving wretched sinners, we must humbly accept the gift of His salvation.


JUMANNE TAREHE 8 DESEMBA 2020    ASUBUHI                   

MITHALI 8:22-27

22 Bwana alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake, Kabla ya matendo yake ya kale.
23 Nalitukuka tokea milele, tangu awali, Kabla haijawako dunia.
24 Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa, Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji.
25 Kabla milima haijawekwa imara, Kabla ya vilima nalizaliwa.
26 Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde Wala chanzo cha mavumbi ya dunia;
27 Alipozithibitisha mbingu nalikuwako; Alipopiga duara katika uso wa bahari;

Mwana wa Mungu anajishuhudia mwenyewe kuwa alihusika katika kazi ya uumbaji. Hata dunia ilipoharibika, alifanyika mwokozi wa ulimwengu, yeye mwenyewe aliyeumba. Mwana wa Mungu aliwekwa wakfu na Mungu, kabla ya misingi ya dunia kuwako, kwa ajili ya kazi hii kuu ya ukombozi. Ikiwa Kristo anapendezwa kuwaokoa wenye dhambi, tunahitaji kuipokea zawadi hiyo ya wokovu kwa unyenyekevu.