Date: 
17-03-2021
Reading: 
Philippians 4:15-20

WEDNESDAY 17TH MARCH 202!   MORNING                                     

Philippians 4:15-20  New International Version (NIV)

15 Moreover, as you Philippians know, in the early days of your acquaintance with the gospel, when I set out from Macedonia, not one church shared with me in the matter of giving and receiving, except you only; 16 for even when I was in Thessalonica, you sent me aid more than once when I was in need. 17 Not that I desire your gifts; what I desire is that more be credited to your account. 18 I have received full payment and have more than enough. I am amply supplied, now that I have received from Epaphroditus the gifts you sent. They are a fragrant offering, an acceptable sacrifice, pleasing to God. 19 And my God will meet all your needs according to the riches of his glory in Christ Jesus.

20 To our God and Father be glory for ever and ever. Amen.

If you want your heart to be with the Lord, put your treasure in the Lord’s work. Giving generously takes faith because you have to trust that when you give away your possessions, God is going to provide for your immediate needs. 


JUMATANO TAREHE 17 MACHI 202I   ASUBUHI                       

WAFILIPI 4:15-20

15 Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.
16 Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja.
17 Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.
18 Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
20 Sasa atukuzwe Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina.

Ikiwa unataka moyo wako uwe kwa Bwana, weka hazina yako katika kazi za Bwana. Kutoa kwa moyo kunahitaji imani kwa sababu unapaswa kuamini kuwa unapotoa mali zako, Mungu atakupa mahitaji yako yote.