MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 30 APRILI, 2017
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI YESU KRISTO NI MCHUNGAJI MWEMA
- Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
- Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti.
- Kamati ya Misioni na Uinjilisti kwa niaba ya Uongozi wa Kanisa Kuu Azania Front, inapenda kuwatangazia watu wote kuwa leo ndio siku ya mwisho ya Semina ya NDOA NA FAMILIA iliyoanza jumamosi tarehe 22.04.2017. tunamshukuru sana Mungu kwa kutuwezesha kuwa na Semina hii na kumruhusu mtumishi wake Mch. Mathias Mushi na Mkewe Jessie Mushi kuihudumia semina hiyo kwa mafundisho, ushauri na maombi. Tunawapongeza sana wote walioweza kufika ikiwa ni watoto, vijana, wajane, wagane na wanandoa. Tunajua mbegu iliyopandwa katika semina hii kwa wale waliolipokea neno itaota na kukua na kuzaa matunda yampendezayo Mungu. Mungu awabariki sana. Kipindi cha leo kitaanza saa 10.00. Aidha siku ya alhamisi tarehe 04.05/2017 saa 11.30 jioni kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi. Wote mnakaribishwa.
- Ukarabati wa vioo vya madirisha ya Kanisa kuu ambao ulifadhiliwa kwa kiasi furani na ubalozi wa ujerumani hapa Dar es Salaam umekamilika. Na sasa vioo vyetu vimekaa vizuri kama mnavyoona vinapendeza.
- NDOA
NDOA ZA WASHARIKA
Kwa mara ya Kwanza tunatangaza ndoa za tarehe 13/05/2017
SAA 8.00 MCHANA
Bw. Salim Athuman Kisuda na Bi. Sarah Laili Mussa
SAA 10.00 JIONI
Bw. Nzota Gideon Killango na Bi. Margareth Frank Mtui
Kwa mara ya Pili tunatangaza ndoa za tarehe 13/05/2017
SAA 9.00 ALASIRI
Bw. Erick Godian Mwakipesile na Bi. Adeline Josephine Mmbaga
SAA 10.00 JIONI
Bw. Ajelandro Mushobozi Sindano na Bi. Rehema Mahmoud Kikwere
Kwa mara ya Tatu tunatangaza ndoa za tarehe 06/05/2017
SAA 6.00 MCHANA
Bw. Morries Walter Shangali na Bi. Elke Norah Sumari
SAA 10.00 JIONI
Bw. Eliah Emmanuel Kinyunyu na Bi. Emilia Bonifas Mdamba
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.
- Ibada za Nyumba kwa Nyumba
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Ndosi
- Kinondoni: Kwa Prof. na Bibi Kulaba
- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watatangaziana
- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watatangaziana
- Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
- Tabata: Watatangaziana
- Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Mama Ruth Korosso
- Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Stanley Mkocha
- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Dk na Bibi Kinasha