MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 08 JANUARI, 2017
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI: WABATIZWAO NDIO WANA WA MUNGU.
- Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
- Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti:
- Ibada ya Maombi na maombezi leo haitakuwepo mpaka tarehe 26/01/2017.
- Wazazi na Walezi wenye watoto wanaoanza Kipaimara mwaka wa Kwanza 2017 wafike ofisi ya Parish Worker ili wajiandikishe.
- Jumamosi ijayo tarehe 14/01/2017 kutakuwa na ibada ya pamoja ya nyumba kwa nyumba (jumuiya) zote kwa kuanza mwaka mpya wa 2017. Ibada hii itaanza saa 2.00 asubuhi. Wote mnaombwa kuhudhulia ibada hii muhimu.
- Jumapili ijayo tarehe 15/01/2017 katika ibada ya pili, walimu wa shule ya jumapili watamshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyowatendea na kuwavusha mwaka 2016 salama na kuingia mwaka 2017.
Neno: Zab. 134:1-3,
Pia familia ya Dr. Lema nao watamshukuru Mungu tarehe 15/01/2017 katika ibada ya pili kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na Uponyaji wa Mama Rachel Lema.
Neno: Zab. 121:1-8, Wimbo: 295
- NDOA:
Matangazo ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu