Hii ni Pasaka;
Jumatano asubuhi tarehe 06.05.2026
Ufunuo wa Yohana 15:2-4
2 Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.
3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.
4 Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
Njooni tumsifu Mungu wetu;
Yohana anafunuliwa na kuona watu wanaomsifu Mungu. Wanauimba wimbo wa Musa, na ule wa Mwana kondoo wakisema matendo ya Bwana ni makuu na ya ajabu, njia zake ni za haki, yeye aliye mfalme wa mataifa.
Uhai tulio nao, na wokovu tuliopewa bure kwa kufa na kufufuka kwa Yesu msalabani, ni matendo makuu yanayotupa sababu ya kumsifu Mungu. Tumpe sifa maana anastahili. Sifa njema kuliko zote ni kuishi kwa kadri ya mapenzi yake. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
