Hii ni Pasaka;
Jumamosi asubuhi 02.05.2026;
Warumi 15:7-13
7 Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe.
8 Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;
9 tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.
10 Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na watu wake.
11 Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana; Enyi watu wote,mhimidini.
12 Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini.
13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Ndani ya Kristo tunakuwa wapya;
Paulo anahubiri upendo akiwataka watu wa Rumi kukaribishana wao kwa wao kama Kristo alivyowakaribisha waliompokea. Kristo ndiye utimilifu wa Agano la Mungu, astahiliye kutukuzwa, hivyo anawataka Warumi kumtukuza Kristo kwa maisha yao yenye upendo kwa Mungu na watu.
Ujumbe wa Paulo ulikuwa watu wa Rumi kuishi kwa ukarimu, kwa mfano wa Kristo aliyewaita wakipendana na kukaribishana wao kwa wao. Ni ujumbe unaokuja kwetu asubuhi ya leo, ukitutaka kuishi kwa upendo, kama Yesu mfufuka anavyotuagiza maana upendo ni amri itokayo kwake. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
