DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 15 MACHI, 2026
SIKU YA BWANA YA 3 KABLA YA PASAKA
NENO LINALOTUONGOZA NI
YESU NI CHAKULA CHA UZIMA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 08/03/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 08/03/2026 ni Washarika 758.
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Jumatano ijayo tarehe 18/03/2026 saa 11.00 jioni tutaendelea na ibada ya Kwaresma. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu.
8. Jumapili ijayo tarehe 22/03/2026 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.
9. SHUKRANI: Jumapili ijayo tarehe 22/03/2026 katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi
- Familia ya Bwana na Bibi Lazaro Kibiwi watamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mkewe Neema 22/3/
Neno: Zaburi 139:14
10. Jumamosi ya tarehe 11/04/2026 kutakuwa na ibada ya wazee kuanzia miaka 65 ambayo itaambatana na Meza ya Bwana. Wazee wote wanaombwa kujiandaa kuhudhuria ibada hiyo. Wale ambao watakuwa na changamoto ya usafiri wafike ofisi ya Mchungaji ili waweze kuwezeshwa kufika katika ibada hiyo. Washarika tuendelee kuiombea ibada hiyo.
11. Jumapili ya tarehe 12/04/2026 katika ibada zote tatu tutampongeza Mch. Charles Mzinga pamoja na familia yake kwa kipindi alichotumika hapa Kanisa Kuu Azania Front. Jumuiya zote, Vikundi vyote na Washarika wote mnaombwa kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo. Mungu awabariki.
12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Upanga: Kwa Bi Agnes Mziray
- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Korosso
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Moses Kombe
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni:, Oysterbay na Masaki:, Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach:, Watashiriki ibada hapa Kanisani
13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
