Date:
28-01-2025
Reading:
Luka 8:19-21
Hii ni Epifania
Jumanne asubuhi tarehe 28.01.2025
Luka 8:19-21
19 Wakamwendea mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano.
20 Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe.
21 Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.
Mungu hana upendeleo;
Yesu alikuwa katikati ya makutano akifundisha, mara mama yake na ndugu zake walifika wakitaka kuonana naye. Walituma watu kumuita maana wasingemfikia kwa sababu ya umati mkubwa. Jibu la Yesu lilikuwa la kushangaza, akisema "..mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya".
Baadhi hufikiri Yesu labda hakuwa karibu na ndugu zake, hakuwapenda, aliwadharau. Ukweli ni kuwa Yesu alikuwa anajitambulisha kama Mesiya, Mwokozi wa ulimwengu. Alitaka watu wasimuone kama ndugu tu wa jamaa yake, bali Kristo. Yesu alipojitambulisha na kusema walisikiao neno lake ndiyo ndugu zake hakuonesha upendeleo, maana aliwaita wote. Hata sasa anatuita wote kwake bila upendeleo, mwamini sasa uokolewe. Amina
Jumanne njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
bernardina.nyamichwo@gmail.com