Date:
27-01-2025
Reading:
1 Yohana 16-18
Hii ni Epifania
Jumatatu asubuhi tarehe 27.01.2025
1 Yohana 4:16-18
16 Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
17 Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.
18 Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
Mungu hana upendeleo;
Yohana anaandika juu watu kupendana maana pendo latoka kwa Mungu ambaye alitupenda kwanza. Kwa njia ya imani tumelifahamu pendo la Mungu, kwamba mwenye pendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. Pendo la Mungu halina hofu maana latoka kwake, yaani hilo pendo likitujaa moyoni hofu inaondoka kwetu.
Ujumbe wa Yohana ni sisi kupendana kama Kristo alivyotupenda, yaani tuuige mfano wake wa upendo. Kusema tunampenda Mungu wakati hatupendani sisi kwa sisi ni uongo kama Yohana anavyendelea kuandika kwenye waraka wake;
1 Yohana 4:20-21
20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. 21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.Tuache upendeleo, tupendane. Amina
Uwe na wiki njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650