Date: 
24-01-2025
Reading: 
Mwanzo 36:1-6

Hii ni Epifania 

Ijumaa asubuhi tarehe 24.01.2025

Mwanzo 39:1-6

1 Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko.

2 Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.

3 Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake.

4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.

5 Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.

6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.

Mungu hubariki nyumba zetu;

Asubuhi hii tunasoma Yusufu anauzwa na Waishmaeli kwa Potifa, akida wa Farao. Tunasoma kwamba Bwana alikuwa na Yusufu, akastawi na kufanikiwa. Yusufu akaona neema ya Mungu, akamtumikia. Ilitokea Yusufu akawekwa kuwa msimamizi wa vitu vyote kwenye nyumba ya Potifa, na Bwana akaibariki nyumba ya yule akida wa Farao. 

Tunaona Yusufu akimtumikia Mungu kwa kuona neema yake, na Yusufu anafanywa mkuu katika nyumba aliyouzwa. Mbaraka wa Bwana ulikuwa juu ya vyote vilivyokuwa kwenye nyumba ile na shamba. Yusufu akaachiwa kila kitu na Bwana wake. Utume na uaminifu wa Yusufu ulimfanya kubarikiwa yeye na nyumba ya Potifa. Nasi tukimwamini Yesu anabariki nyumba zetu. Amina

Ijumaa njema

 

Heri Buberwa 

Mlutheri