Date:
22-01-2025
Reading:
Luka 8:40-42
Hii ni Epifania
Jumatano asubuhi tarehe 22.01.2025
Luka 8:40-42
40 Basi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana walikuwa wakimngojea wote.
41 Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake;
42 kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.
Mungu hubariki nyumba zetu;
Somo la leo asubuhi ni sehemu ya habari ya Yairo aliyekuwa ofisa mkuu wa Sinagogi mwenye heshima na kufahamika. Huyu alikuja kwa Yesu kuomba amponye binti yake akiwa amekata tamaa, lakini akitafuta jinsi ya kunusuru maisha ya mtoto wake. Yesu hakuwepo kwa wakati unaoonekana ulikuwa muafaka kwa uponyaji wa yule mtoto, alikuwa amevuka bahari, na alikuwa hajarudi.
Aliporudi alianza kumponya mwanamke aliyekuwa akitokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili. Ndipo akamfufua binti Yairo ambaye alikuwa tayari amekufa. Tukio hili lilishangaza wengi, maana hata Yesu aliposema mtoto amelala, walimcheka. Yairo alimwamini Yesu, naye Yesu akaibariki nyumba yake. Nasi tukimwamini Yesu anabariki nyumba zetu. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa