MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 19 JANUARI, 2025
SIKU YA BWANA YA 2 KATIKA MAJIRA YA UFUNUO
NENO LINALOTUONGOZA NI
MUNGU HUBARIKI NYUMBA ZETU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia kwa cheti:
3. Matoleo ya Tarehe 12/01/2025
4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
5. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 12/01/2025 ilikuwa ni washarika 751. Sunday School 102
6. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
7. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
8. Uongozi wa Usharika unapenda kuwataarifu kuwa mafundisho ya watoto wa Kipaimara mwaka 2025 kwa kiswahili yameanza jana Jumamosi tarehe 18/01/2025 saa 3.00 asubuhi hadi saa 5.00 asubuhi. Mafundisho ya Kingereza yataanza jumamosi ijayo tarehe 25/01/2025. Wazazi mnaombwa sana ushirikiano wenu.
9. Kwaya ya AGAPE, wanatarajia kwenda kuwatembelea watoto wenye tatizo la mgongo wazi katika hospitali ya Taifa - Muhimbili, pamoja na watoto wenye uhitaji wanaolelewa katika kituo cha watoto KIBAHA CHILDREN VILLAGE CENTRE mkoa wa Pwani, January 2025. Kila mwaka kwaya ya Agape hutoa huduma hii na wanapenda kuwashukuru sana washarika wote waliojitoa kwa ajili ya huduma iliyopita. Hivyo wanaomba sana washarika kuwaunga mkono kwa kuchangia huduma hiyo. Unaweza kuchangia fedha taslimu, nguo, mafuta ya ngozi, sabuni za kufulia na kuogea, madaftari, kalamu, maji ya kunywa, dawa za meno au chochote utakachobarikiwa na Mungu. Tafadhali wasilisha sadaka yako ofisi ya Usharika au unaweza kutuma sadaka yako kupitia Account no. 3874006021 jina AGAPE EVANGELICAL SINGER AZANIA FRONT Maendeleo Bank. Mungu wa Mbinguni awabariki sana.
10. SHUKRANI: TAREHE 26.01.2025 KATIKA IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI
- Wagane na Wajane Azania Front watamtolea Mungu Sadaka ya Shukrani kwa mambo makubwa aliyowantedea. Baada ya ibada hiyo kutakuwa na kikombe cha chai.
IBADA YA TATU SAA 4.30
- Walimu wa shule ya jumapili watamshukuru Mungu kwa kuwalinda, kuwatunza na kuwapigania kwa kipindi chote cha mwaka jana na kuona mwaka wa 2025.
Neno: Zab. 92:1, Wimbo: TMW 264
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mathias Kavugha
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Peter Mlagha
- Mjini kati: Watafanyia hapa kanisani saa 1.00 asubuhi.
- Mikocheni, Kawe na Mbezi Beach: kwa Prof Esther Mwaikambo.
12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.