Date: 
21-01-2025
Reading: 
2 Samweli 7:27-29

Hii ni Epifania 

Jumanne asubuhi tarehe 21.01.2025

2 Samweli 7:27-29

27 Kwa kuwa wewe, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli umenifunulia mimi, mtumwa wako, ukisema, Nitakujengea nyumba; kwa hiyo mimi, mtumwa wako, nimeona vema moyoni mwangu nikuombe dua hii.

28 Na sasa, Ee Bwana MUNGU, wewe ndiwe Mungu, na maneno yako ndiyo kweli, nawe umemwahidia mtumwa wako jambo hili jema

29 basi, sasa, uwe radhi, ukaibarikie nyumba ya mtumwa wako, ipate kudumu milele mbele zako; kwa maana wewe, Ee Bwana MUNGU, umelinena na kwa baraka yako nyumba ya mtumwa wako na ibarikiwe milele.

Mungu hubariki nyumba zetu;

Bwana Asifiwe;

Katika sura ya tano, Daudi anapakwa mafuta kuwa Mfalme wa Israeli. Yerusalemu panafanywa makao makuu, na Wafilisti wanaivamia Israeli lakini shambulizi lao linazimwa. Sura ya 6 Daudi analeta sanduku la Agano Yerusalemu, anafanya sherehe kubwa na kumtolea Bwana sadaka. Anawaongoza watu kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa kama shukrani kwa Bwana.

Sura ya 7 sasa Bwana anaweka agano na Daudi. Anamuahidi kuwa naye katika Ufalme wake, hata kufa kwake. Isome kwa ufupi ahadi ya Bwana kwa Daudi;

2 Samweli 7:8-9

8 Basi, sasa, mwambie mtumishi wangu, Daudi, maneno haya, Bwana wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli;
9 nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani.

Ahadi ya milele anampa pia;

2 Samweli 7:11-12

11 naam, kama vilivyokuwa tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi, wawe juu ya watu wangu Israeli; nami nitakustarehesha mbele ya adui zako wote. Tena Bwana anakuambia ya kwamba Bwana atakujengea nyumba.
12 Nawe siku zako zitakapotimia, ukalala na baba zako, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake.

Baadaye Daudi anamuomba Mungu aliye Mkuu kuifanya imara nyumba ya Daudi, yaani kuusimamisha na kuuimarisha Ufalme wake katika Israeli. Daudi alijua kuwa alipewa ufalme na Bwana, hivyo anaomba Bwana awe naye katika ufalme wake (18-26)

Ndipo katika somo la leo asubuhi Daudi anaomba baraka ya Bwana ili nyumba yake idumu milele, kama ahadi ya Bwana ya baraka yake kudumu milele ilivyo. Nasi tumtumikie Mungu wetu ili abariki nyumba zetu. Amina

Jumanne njema

Heri Buberwa