MATANGAZO YA USHARIKA  

TAREHE 08 DECEMBA, 2024

SIKU YA BWANA YA PILI KATIKA MAJILIO (ADVENT)

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

UKOMBOZI WETU UMEKARIBIA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 01/12/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei yaTsh. 40,000/=. 

6. Uongozi wa umoja wa Vijana Azania Front unapenda kuwatangazia vijana wote kuwa kutakuwa na mkutano mkuu wa umoja wa vijana siku ya jumapili tarehe 15/12/2024 kwanzia saa 3 :30 Asubuhi hadi saa 6:00 mchana, vijana wote mnahimizwa kushiriki .

7. Jumapili ijayo tarehe 15/12/2024 katika ibada ya kwanza familia ya Pamela unyo na Anitha Raymos watamtolea Mungu shukrani ya pekee kwa mambo mengi Mungu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na uponyaji kwa afya zao. Neno Zaburi 103:1-5

8. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 28/12/2024 ITAKAYOFUNGWA KKKT AZANIA FRONT KATI YA 

  • Bw. Yusuph Elieza Lazalo na Bi Ainess Solomon Seythiel

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu. 

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Bi Agness Mziray
  • Mjini kati: Kwa ……………………………………
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bw & Bi Munisi    
  • Kinondoni: Kwa …………………………………………
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw & Bi Albert Olotu
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bw & Bi Kenneth Mawere
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bi Itemba
  • Oysterbay, Masaki: Kwa Bw & Bi Desmond Mushi

10. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la KWANZA  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.