MATANGAZO YA USHARIKA  

TAREHE 01 DECEMBA, 2024

SIKU YA BWANA YA KWANZA KATIKA MAJILIO (ADVENT)

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

BWANA ANALIJIA KANISA LAKE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 24/11/2024  

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei yaTsh. 40,000/=. 

6. Jumapili ya leo tarehe 01/12/2024 tutamtolea Mungu fungu la kumi.  

7. Jumapili ijayo tarehe 7/12/2424 Katika ibada ya kingereza Familia ya Mr & Mrs Innocent Elisha Ngowi watamshukuru Mungu kwa Mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na binti yao wa kwanza kutimiza miaka 18, Pia kwa wao kutimiza miaka 18 ya ndoa yao Zaburi 52:9 Kumb 28:3.

8. Uongozi wa wanawake dayosisi ya mashariki na Pwani wanapenda kuwajulisha wanawake kuwa maadhimisho ya kristmas yatafanyika siku ya jumamosi tarehe 07/12/2024 katika usharika wa kipawa kwanzia saa mbili asubuhi wanawake mjiandae kushiriki siku hiyo. 

9. Uongozi wa umoja wa Vijana Azania Front unapenda kuwatangazia vijana wote kuwa kutakuwa na mkutano mkuu wa umoja wa vijana siku ya jumapili tarehe 15/12/2024 kwanzia saa 3 :30 Asubuhi hadi saa 6:00 mchana, vijana wote mnahimizwa kushiriki .

10. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 07/12/2024

SAA 8.00 MCHANA

  • Bw. Edward Charles Nyange na Caroline Marco Kasuga

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu. 

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: ……………………………………
  • Mjini kati: Kwa Ndeni Kimaro
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Ruth Korosso
  • Kinondoni: Kwa…………………………………………
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw & Bi Mujuni Mutembei
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa ………………………….
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw na Bi Rweikiza 
  • Oysterbay, Masaki: Kwa Bi Lightness Moshi.

12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la PILI  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki