Date: 
21-11-2024
Reading: 
Amosi 8:1-3

Alhamisi asubuhi tarehe 21.11.2024

Amosi 8:1-3

1 Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, kikapu cha matunda ya wakati wa hari.

2 Akaniambia, Amosii, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa hari. Ndipo Bwana akaniambia, Mwisho wao umewajilia watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe.

3 Tena nyimbo za hekaluni zitakuwa vilio siku ile, asema Bwana MUNGU; mizoga itakuwa mingi; kila mahali wataitupa, wakinyamaza kimya.

Jiandae kwa hukumu ya mwisho;

Nabii Amosi alikemea vitendo viovu kama alivyotumwa na Bwana. Katika somo la asubuhi hii, tunaona Amosi akitoa ujumbe kwa Israeli kumcha BWANA, vinginevyo furaha yao itageuka kilio siku ya mwisho.

Ujumbe huu unatujia asubuhi ya leo, kuwa tusione ambavyo tunafurahia maisha sasa, tusipotubu na kubadilika tutalia machozi siku ya hukumu. Siku njema.

 

Heri Buberwa