Date: 
21-11-2024
Reading: 
Amosi 8:1-3

Alhamisi asubuni tarehe 21/11/2024

Amosi 8:1-3

1 Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, kikapu cha matunda ya wakati wa hari.

2 Akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa hari. Ndipo BWANA akaniambia, Mwisho wao umewajilia watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe.

3 Tena nyimbo za hekaluni zitakuwa vilio siku ile, asema Bwana MUNGU; mizoga itakuwa mingi; kila mahali wataitupa, wakinyamaza kimya.

Jiandae na hukumu ya mwisho.

Ukisoma mitari inayofuata,

4 Lisikieni hili, ninyi mnaopenda kuwameza wahitaji, na kuwakomesha maskini wa nchi,

5 mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na sabato nayo, tupate kuandika ngano? Mkiipunguza efa na kuiongeza shekeli, mkidanganya watu kwa mizani ya udanganyifu;

6 tupate kuwanunua maskini kwa fedha, na wahitaji kwa jozi ya viatu; na kuziuza takataka za ngano.

Utaona haya ni mambo ambayo yanatendeka hata leo, watu kutokutenda haki hususan dhidi ya wanyonge.

Amosi anatutahadharisha kuhusu ya siku ya hukumu. Wale waliokuwa wakandamizaji wa watu maskini wataangamizwa. Tena watakuwa mahali pa maangamizi ya kutisha.

Hivyo tuishi maisha ya upendo na kutenda haki, tukijua hukumu ya Mungu hakika itakuja.

Siku njema.

Mzee Swai.