Date: 
20-11-2024
Reading: 
2Wathesalonike 1:3-10

Jumatano asubuhi tarehe 20.11.2024

2 Wathesalonike 1:3-10

3 Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.

4 Hata na sisi wenyewe twaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya saburi yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.

5 Ndiyo ishara hasa ya hukumu iliyo haki ya Mungu, ili mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa.

6 Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi;

7 na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake

8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;

9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;

10 yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).

Jiandae kwa hukumu ya mwisho;

Mtume Paulo anawaandikia Wathesalonike kuhusu hukumu wakati wa kuja kwa Yesu, akiwakumbusha kuwa hukumu ya Mungu itakuwa ya haki, yaani atamhukumu kila mmoja kulingana na matendo yake. Anaonesha kuwa wasioitii Injili watapata maangamizi ya milele (9).

Tunaepukaje maangamizi ya milele? Kwa kuitii Injili ya Kristo, na kudumu katika utume kama alivyotuita, ili siku akirudi tusiachwe.

Siku njema.

Heri Buberwa