MATANGAZO YA USHARIKA  

TAREHE 17 NOVEMBA, 2024

SIKU YA BWANA YA 2 KABLA YA MAJILIO

NENO LINALOTUONGOZA NI

JIANDAE KWA HUKUMU YA MWISHO

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Wageni Waliotufikia kwa cheti ni Maxwell S. Ng’walida na Makk S. Ng’walida toka Usharika wa Kanisa Kuu Imani KKKT Dayosisi ya Mashariki ya ziwa Victoria Mwanza, Wamekuja masomoni. 

3. Matoleo ya Tarehe 10/11/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei yaTsh. 40,000/=. 

6. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inamshukuru Mungu kwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa Mwaka wa Kwanza na wa pili yaliyofanyika jana jumamosi tarehe 16/11/2024 kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 9.00 alasiri hapa Usharikani. Tunawashukuru pia Wazazi na Walezi. Mungu awabariki.

7. Jumapili ijayo tarehe 24/11/2024 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

8. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 24/11/2024 katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi familia mbili zitamshukuru Mungu

  • Margaret Jim Lema pamoja na familia atamshukuru Mungu kwa maisha ya mume wake, Baba, Kaka na shemeji Mzee Alex Lema, kuugua na kumpumzisha salama.

Neno: Zaburi 23:4, Wimbo: TMW 175, Kwaya kuu (Kimbilio langu ni kwa Yesu Kristo )

  • Familia ya Bwana na Bibi Elisha Mushumbusi watamshukuru Mungu kwa kufanikisha shughuli ya ndoa ya watoto wao Emmanuel na Maureen.

Neno: Efeso 3: 20-21, Wimbo: TMW 262, Kwaya kuu (Vita vya nchi Yesu kashinda)

9. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 07/12/2024

SAA 8.00 MCHANA

  • Bw. Edward Charles Nyange na Caroline Marco Kasuga

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu. 

10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mathew Munisi
  • Mjini kati: itafanyika hapa kanisani jumamosi saa 1.00 asubuhi
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa ……………………………
  • Kinondoni: Kwa …………………………………………
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw Yono na Bi Scholastica Kevela
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Bwana na Bibi Kakuyu
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa …………………………………..
  • Oysterbay, Masaki: Kwa Eng. na Bibi H. Towo.

11. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.