Date: 
14-11-2024
Reading: 
Ufunuo wa Yohana 3:11-13

Alhamisi asubuhi tarehe 14.11.2024

Ufunuo wa Yohana 3:11-13

11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.

12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.

13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka;

Yohana anafunuliwa kurudi kwa Yesu, hivyo kuleta ujumbe wake, kuwa kila mtu ashike alicho nacho asije mwingine kuitwaa taji yake. Ashindaye anaahidiwa kuwa nguzo katika hekalu, yaani kuwa mtu wake hadi uzima wa milele.

Ni ujumbe unaotuita kudumu katika imani, tukiepuka mambo yote yanayoweza kusababisha tukamwacha Yesu (yaani tusishike sana tulicho nacho). Dumu katika pendo na wokovu aliotuletea Yesu kwa ajili ya sasa, kesho na hata uzima wa milele. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa