Date: 
08-11-2024
Reading: 
1 Wathesalonike 3:11-13

Ijumaa asubuhi tarehe 08.11.2024

1 Wathesalonike 3:11-13

[11]Basi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu, atuongoze njia yetu tufike kwenu.

[12]Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;

[13]apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.

Sisi ni wenyeji wa mbinguni;

Mtume Paulo anawatia moyo Wathesalonike wazidi kukaa katika imani, wakiwa na upendo miongoni mwao, kwa mioyo isiyo lawama mbele za Mungu. 

Kama Paulo alivyowaita Wathesalonike, nasi tunaitwa kuishi kwa haki, kwa upendo tukiwa wamoja katika Kristo, ili Bwana akija asituache.

Siku njema

Heri Buberwa