Date: 
07-11-2024
Reading: 
Zaburi 16:1-6

Alhamisi asubuhi tarehe 07.11.2024

Zaburi 16:1-6

1 Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.

2 Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu; Sina wema ila utokao kwako.

3 Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.

4 Huzuni zao zitaongezeka Wambadilio Mungu kwa mwingine; Sitazimimina sadaka zao za damu, Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.

5 Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu.

6 Kamba zangu zimeniangukia mahali pema, Naam, nimepata urithi mzuri.

Sisi ni wenyeji wa mbinguni;

Asubuhi hii tunasoma sehemu ya wimbo wa Daudi, wimbo ambao ni sala akiomba kulindwa na Mungu. Daudi anaomba ulinzi wa Mungu akijikabidhi kwake. Katika sala yake, Daudi anasema wasiomcha Bwana hukaa katika huzuni. Lakini yeye Daudi anajiweka kwa Bwana, akiona yuko kwenye urithi mzuri.

Hii sala tuitafakari kwa kumtazama Kristo, tukiomba ulinzi wake maishani mwetu. Tufahamu kuwa pasipo Kristo ni huzuni tu, bali furaha ya kweli yapatikana kwake. Tuungane na Daudi tukiomba neema ya Mungu isiondoke kwetu, ili tubaki kuwa wenyeji wa mbinguni. Amina

Alhamisi njema 

Heri Buberwa