Date:
29-10-2024
Reading:
Waebrania 10:23-25
Jumanne asubuhi tarehe 29.10.2024
Waebrania 10:23-25
23 Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu;
24 tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;
25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Mwenye haki ataishi kwa imani
Baada ya mwandishi wa waraka kwa Waebrania kuandika kwamba kafara ya Kristo inatosha (10:1-18), sasa anawaita wasomaji wake kuwa wavumilivu katika Kristo Yesu. Anaendelea kuwasihi wasomaji wake kulishika ungamo la tumaini katika Kristo wakihimizana katika upendo na kazi nzuri.
Mwandishi anaendelea kuhimiza kuwa waamini wasiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi, bali waonyane na kutenda yawapasayo wakimngojea Bwana. Ujumbe mkuu ni kudumu katika Bwana tukiwa wavumilivu na kutenda yatupasayo, tunapomngojea Bwana. Amina
Jumanne njema
Heri Buberwa