Date:
18-10-2024
Reading:
Yeremia 17:7-8
Ijumaa asubuhi tarehe 18.10.2024
Yeremia 17:7-8
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.
Ni baraka kuitikia wito;
Yeremia anawapa Taifa la Mungu ujumbe juu ya kumtegemea Bwana, akisema heri amtegemeaye Bwana na kumfanya tumaini lake. Anamfananisha mtu huyu na mti upandwao kando ya maji, huzaa matunda pasipo kukauka.
Ukisoma nyuma kidogo unaona ujumbe wa Bwana kupitia kwa Yeremia kwamba amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu;
Yeremia 17:5-6
5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. 6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.Wito wa Bwana kwetu ni kumtegemea Bwana katika maisha yetu, ili atuongoze na kutupa uzima wa milele. Amina
Ijumaa njema.
Heri Buberwa