MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 01 SEPTEMBA, 2024

SIKU YA BWANA YA 14 BAADA YA UTATU 

NENO LINALOTUONGOZA NI

MPENDE JIRANI YAKO 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 25/08/2024

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wte katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

6. Kitenge chetu cha kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya shilingi 40,000/= 

7. Tarehe 06/10/2024 itakuwa ni sikukuu ya mavuno. Washarika tujiandae na kuiombea siku hiyo. Sare itakuwa ni kitenge chetu cha Kiharaka.

8. Leo tarehe 01/09/2024 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni. 

9. Tarehe 28/09/2024 na 29/09/2024 itakuwa ni sikukuu ya mikaeli na watoto. Hivyo tunaomba vikundi vyote vizingatie sherehe hii muhimu ili tuweze kuwaenzi, kuwatunza na kuwatia moyo watoto wetu kwa kuwachangia chochote ili kufanikisha Sikukuu hii. Mungu awabariki.

10. Jumapili ijayo tarehe 08/09/2024 ni siku ya ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

11. "Umoja wa Vijana Azania Front umeandaa ibada ya mkesha maalum unaoitwa "Night of Praise (Season II)" uliobeba kichwa cha mwaka "Sing His Greatness," Kutoka katika Zaburi 145:3. Mkesha huu utafanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front tarehe 4 Oktoba 2024, kuanzia saa mbili usiku hadi alfajiri. Vikundi mbalimbali vya uimbaji vitashiriki, pamoja na paneli ya majadiliano kuhusu afya ya akili (Mental Health), na matukio mengine ya kipekee. Tshirt maalumu kwa hiyo siku zitapatikana wiki ijayo, Wote mnakaribishwa.

12. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

Hakuna ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Mama Gembe.
  • Mjini kati: Mama Kabezi
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Watatangaziana
  • Kinondoni: Kwa Profesa Geofrey Mmari
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi George Msuya
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa ……………………..
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: …………………………. 
  • Oysterbay, Masaki: Kwa………………………

14. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza. 

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.