Date:
08-08-2024
Reading:
Mathayo 11:16-19
Alhamisi asubuhi tarehe 08.08.2024
Mathayo 11:16-19
16 Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema,
17 Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.
18 Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.
19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Enendeni kwa hekima;
Yesu alikuwa anamsifu Yohana Mbatizaji aliyeleta ujumbe wa ujio wa Kristo kama Mwokozi wa ulimwengu, ambaye wapo ambao hawakumuamini. Yesu alikuwa anawaambia
kuwa Yohana alileta habari zake (Yesu) naye Yesu alileta habari za Ufalme wa Mungu ambao unatekwa na wenye nguvu. Katika somo Yesu anawafananisha wasioamini na watoto wakaao sokoni, wakaitwa pasipo kuitika. Yaani hawakuamini ujumbe ya Yohana Mbatizaji, wala hawakumwamini Yesu Kristo.
Tunaposikia neno la Mungu pasipo kuamini tunakuwa sawa na watoto wakaao sokoni wakapigiwa filimbi na wenzao wasicheze, wala wasilie na wenzao. Yaani tunafanana na wale ambao hawakumwamini Yesu. Kumbe njia sahihi katika uanafunzi wetu ni kumwamini Yesu, kumpokea na kumfuata. Basi tudumu katika Imani kama tulivyompokea, sasa na siku zote. Amina
Nanenane njema
Heri Buberwa