Date: 
06-07-2024
Reading: 
Mithali 7:1-3

Jumamosi asubuhi tarehe 06.07.2024

Mithali 7:1-3

1 Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako.

2 Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.

3 Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

Ninyi ni barua ya Kristo;

Mithali za Suleimani zinasomeka katika mtindo wa baba anayeongea na mtoto wake. Katika sura hii ya 7, ni wito kwa mtoto kushika maneno na amri za baba yake. Hapa mkazo mkubwa unaonekana kuzishika amri, zitokazo kwa baba.

Mkazo uliopo ni utii. Angalia sura ya 7 inavyomalizika;

Mithali 7:24-27

24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.
25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.
26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa.
27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.

Kristo ndiye Baba yetu, sisi kama watoto wake. Hivyo anatukumbusha kumwamini, kulishika neno lake na kuishi maisha yanayompendeza. Kutomwamini Yesu ni njia ya kwenda kuzimu (27) maana yeye ndiye njia ya uzima. Mwamini sasa na utende kwa njia ya neno lake. Uwe barua ya Kristo. Amina

Jumamosi njema 

Heri Buberwa